Windows

LightBlog

Monday, February 12, 2018

Vitu 10 Vya Fashion/Urembo Ambavyo Kila Mwanamke Anatakiwa Kuwa Navyo



small walk in closet ideas for women
Katika pitapita zangu mitandaoni hivi leo, hususani Fashion Blogs, nimekutana na posts mbalimbali zinazozungumzia na kuorodhesha vitu mbalimbali ambavyo mwanamke yeyote anayejali au kupenda masuala ya Fashion na Urembo anapaswa kuwa navyo.
Ghafla nikajikuta nawaza vitu ambavyo mimi binafsi ninavyo au nahisi ni muhimu kila mwanamke kuwa navyo. Nikaona basi kwanini nami nisiwe na orodha yangu na kukushirikisha wewe msomaji ? Najua wanawake tunaweza kutofautiana sana linapokuja suala la fashion nk.Tofauti zinaweza kutokana na umri,makazi na hata hali ya hewa. Of course suala la kipato linachangia pia. Mwisho nitakupa nawe nafasi ya kunijulisha kupitia kisanduku cha maoni (comments) au mitandao ya jamii nk.
Sasa kama nilivyosema hapo juu, tastes na priorities zinatofautiana. Kwa hiyo katika orodha hii nitajitahidi kuweka vile vitu ambavyo naona ni “must have” kwa kila mwanamke. Orodha hii sio timilifu (exclusive) lakini hii hapa ni orodha yangu;
Shoes.jpg
  1.  Shoes/Viatu. (Classic Pump, Runners & Sandals): hapa mpaka najionea aibu. Bado niko kwenye mtihani mkubwa sana. Kama kuna therapy nahitaji. Nina ka-ugonjwa ka kupenda viatu. Ila kwa leo ngoja tu niseme aina hizi za viatu ambavyo ninaamini kila mwanamke ni muhimu akawa navyo. Nimeviweka hapa kwa sababu naamini hivi vinaweza kuvaliwa katika matukio mbalimbali. Kuna vingi sana ambavyo lazima uwe navyo kutokana na hali ya hewa, kama boots, (moja ya viatu nivipendavyo) lakini ooh well, nimeona niweke aina hizi tatu, kama nilivyowaambia hapo awali.Mnisamehe tu nina ka-ugonjwa.Nikianza hapa  siwezi maliza. Hebu tuanze tu na hivi; (kuna siku ntaandika topic nzima ya viatu tu)
alicia-keys
A great suit/jumpsuit; Kwangu mimi mwanamke akivaa a good tailored suit(Iliyopimwa hasa) naamini anapendeza sana. Anakuwa kwenye class ya peke yake. Cha muhimu ni kuzingatia suit inakukaa vizuri. Vipimo vyako hasa, kwani suit ikiwa ndogo matatizo na ikiwa kubwa ndio kabisa mchakamchaka. Mimi napendelea zaidi suit ya suruali zaidi ya sketi but kila mtu ana chaguo lake. Muhimu ni kuhakikisha inakutosha na kukukaa vizuri.

Watches.jpg
3: Saa (Beautiful/big Watch); Saa ni mojawapo ya vitu muhimu sana kwangu, sio specific kwa muda. Ooh well; yaah “tuseme kwa muda”.  Mimi natumia saa zaidi  kama sehemu ya jewelry. Kwangu kutoka ndani bila saa mkononi naona kama kitu kime-miss.Ukiichukulia saa kama part ya jewerly yako, lazima utanunua saa ya maana. Saa ninazozipenda zaidi hivi sasa ni Ebel, Movado and Ferragamo.

Perfumes.jpg
4. Manukato/perfume/A personal Scent.  Muda kidogo kulikuwa na mfanyakazi mwenzangu mmoja alikuwa anapenda sana perfume/ manukato. Kila akiingia kazini  ananukia tofauti na harufu kali sana badala ya kunukia zilikuwa zinanuka. Zaidi ya hapo alikuwa anatumia perfume za ghali sana, mwenyewe alikuwa anaamini kabisa perfumes nzuri ni zile ambazo ni ghali zaidi. Na upande mwingine nina rafiki yangu mmoja yeye yuko makini sana na perfumes, na ana aina nyingi sana za perfumes. Mnaweza kaa kwenye duka la perfume masaa na masaa anatafuta perfume. Mpaka ilikuwa tukienda shopping lazima tukubaliane hamuingii duka lolote linalouza manukato. Kuna siku nikamuuliza hivi ni nini hasa wewe na perfumes? Ndipo aliniponifungua macho na kunifundisha siri ya harufu;  lazima ujue na uwe unajua hasa harufu ya mwili wako kabla ya kujua aina gani za perfume zinaendana na hiyo harufu yako, ambayo ni peke yako unayo.  Kuweza kujua ni zipi za kununua ili uwe na aina ya harufu yako pekee  kwenye perfume tofauti. (siku nitazungumzia hapa jinsi ya kujua harufu yako ya mwili, ni topic ya peke yake) Baada ya kujua haya natamani kujua yule mfanyakazi mwenzangu yuko wapi, ili tusaidiane kutokunukisha watu  na nina maana”KUTONUKISHA” watu na harufu za perfumes ghali.
Anyways ndio nikaja kujua na kuwa muangalifu sana katika kuchangua perfumes zangu. Sasa hivi nikitafuta perfumes, lotion, au mafuta ya mwili (Body butter) najua ni harufu gani inaendana na harufu ya mwili wangu. Sasa hivi napendelea  Dior J’Adore L’or Essence De perfume, Narciso Rodriguez for her na  Jo Malone ‘Tuberose Angelica’ Cologne Intense.(ambazo zote nikitumia zinaendana na harufu ya mwili wangu, lakini baada ya miezi ijayo naweza kuwa na list tofauti hapa) Tafadhali usiogope muuliza nduguyo, partner wako au rafiki yako, usije kuwa unawanukia wengine, mwenyewe unajiona baaab kubwa, kumbe sio.
Bags2.jpg
5. Handbag (forever bag):  Handbags nnazo zizungumizia hapa  ni handbags ambazo ukitoka cha kwanza unachofikiria ni kulibeba. Handbag ambayo inaendana na kila outfit. Ile handbag watu wanakuona unairudia kama ndio only bag ulilonalo kumbe ni bag ambalo linaenda na ku fit kila occasion.  Kwangu mimi ni bag simple lakini classy na ambalo linabebaka kila sehemu na uingiza kila makorokoro yetu. Wanawake tunajijua na makorokoro au sio??
Mara nyingi nimejiona na bags za aina ya Hobo, Tote, and Satchel. Nakuwaga nazo mpaka najistukia, wakati mabegi mengine nnayo yamejaa na sijawahi hata kuyavaa. Lakini usiniambie niache nunua handbag, utaua.Nina moja ambalo kuna siku litaniambia limechoka. Aina hizi  tatu za bags naamini kila mwanamke sharti awe nalo au  japo hata  moja wapo.
VITO.JPG
6. A jewelry ambayo haivuliwi. Hii inamhusu kila mtu. Ntajiongelea mimi kwanza.Sasa hivi nimeolewa kwa hiyo nina pete ya ndoa na pete ya uchumba, ambazo zinavaliwa kila siku no matter what. Nilivyokuwa msichana (Kigoli), nilikuwa na earings(hereni) ambazo ilikuwa hata iweje nalala nazo na kuamka nazo. Nilipewa na marehemu bibi yangu. Hivi sasa nabadilisha hereni mara kwa mara, nimekua atii, na nna hereni nyingi lazima zivaliwe, lakini bado zile hereni za bibi nikizivaa naweza pitiliza weeks zimekaa sikioni. Sasa wewe mwenzangu ukijiangalia hapo aidha umeolewa, umechumbiwa, umeahidiwa au hata kama ni single lady, jiangalie utakuwa na aina moja ya jewelry ambayo unalala nayo na kuamka nayo. Inawezekana ikawa ni hereni, mkufu, pete nk ambayo ina maana kubwa kwako na kwa maisha yako. Hiyo naamini kuwa kila mwanamke anayo na kama hana afikirie atagundua alikuwa nayo au anayo sehemu. Hizi tatu sio zangu specifics, kasoro pete, lakini nina watu wangu wa karibu sana ambao hawavui kati ya hizo mbili.( Wenyewe watu wa Mungu, na kila mmoja ana imani yake)
Blazer
6. Blazer. Inapokuja kwenye nguo Blazer kwa Mwanamke ni kama sukari kwenye chai. Uzuri wa blazer ni kwamba inaokoa katika hali au matukio mengi sana. Kwa mfano; kuna wale mbao hawapendi mikono yao ionekane, kuna wale wasiopenda kuvaa full suit, kuna wale ambao wanataka kuonekana proffesional or classy katika situation fulani, kuna wale wanaosikia baridi maofisini n.k.  Katika matukio yote hayo, Blazer inakuokoa.. Mimi ni mmoja wa wapenda Blazers. Naamini ni kitu ambacho ni muhimu sana kila mwanamke awe nayo. Uzuri  kuna aina nyingi sana za blazers za kuvalia chochote kuanzia  kwenye sketi, jeans mpaka gauni.  Kuwa mwangalifu, lakini kwa aina hizi tatu nina uhakika hutokosea.
Lips
7.  Lip Gloss /Lip balm/Lipstick. Topic au mada ya masuala ya make up  ni kubwa sana. Ukizungumzia make up inahusu vitu vingi, kuna wale ambao hawaondoki nyumbani bila kupaka makeup.Kuna wale ambao make up sio big deal sana katika maisha yao labda kama  kuna mahali muhimu wanaenda. Wao wanaopenda kuwa natural. Leo nitazungumzia kipande kidogo cha idara nzima ya make-up.
katika aina zote za wanawakwe niliowaandika hapo juu, wote hawa watakwambia lazima  wana aidha  lipticks au lipgloss. Mimi ni wale wa lipgloss. Haikai mbali. Lipsticks huwa natumia lakini mara chache na kwenye shughuli maalumu. Kwahiyo  ndio maana imeingia kwenye hii orodha yangu kwa sababu ni kitu ambacho naamini ni muhimu kwa mwanamke kuwa nacho.Lips muhimu sana jamani,  chop lips (midomo iliyokauka)  kwa kweli haipendezi kwa mwanamke, hii mwenzangu hata kwa wanaume. oops nimetoka nje ya topic eeh, anyways imebidi nichomokee hapo. Haya tuendelee, Aina hizi tatu ndizo ninazozipenda zaidi;
Black Dress
8. Little Black Dress(Kigauni Cheusi): Hili kwa kweli sijui kama kuna mwanamke ambae hana gauni jeusi. Umuhimu wake haulezeki. Ni kimbilio la wengi hasa wakati unaposema hujui cha kuvaa. Little black dress is always there to save the day. Ukinenepa, ukikonda, ukiwa unataka kuvaa viatu ambavyo haviendani na kitu, na mengine mengi. Hebu jiangalie una Black Little Dresses ngapi kwenye kabati lako?

Jeans.jpg
9: Pair of Fitted Jeans( Jeans inayokukaa Haswaa)  Hakuna kitu kigumu kama kununua jeans. Japokuwa ukiangalia ni kitu ambacho wengi wanavaa. Kwangu hata siku moja sijawai kununua jeans online(kwa mfano). Naamini kwamba Jeans lazima uijaribu, na sio kila jeans kila mtu anaweza kuvaa. Ni muhimu ujue shape yako na aina ya jeans ambayo inaendana na mwili wako.
Jeans, kama ambavyo bila shaka wote tunakubaliana, ni kitu muhimu sana. Ni miongoni mwa vitu ambavyo sharti viwepo kwenye closet. Ukipata muda jaribu kutafuta historia ya jeans uisome. Hivi sasa jeans ni aina moja ya nguo ambayo inavaliwa katika sehemu mbalimbali,matukio mbalimbali na kwa style tofauti tofauti
Kwa kutumia hawa celebrities hapo juu nimeonyesha jinsi mimi binafsi hupenda kuvalia vazi la jeans.
Miwani.jpg
10.Sun Glasses. Kuna wakati nilikuwa navaa sunglasses kama fashion tu. Yes najua ni moja ya fashions statement. Hata hivyo ninavyozidi kukua sunglasses imekua kitu muhimu sana katika maisha yangu hususani wakati wa mchana.
Pia nimegundua ni kitu kingine ambacho nakinunua mara kwa mara. Zamani nilikuwa sijali sana aina ya miwani. Nilikuwa nanunua tu.  Hivi sasa nimeona umuhimu wa kuwekeza kwenye miwani. Kuna tofauti kubwa sana katika suala zima la muonekano na jinsi inavyolinda macho yako kutokana na miale au mionzi ya jua. Bila shaka unajua aina nyingi za miwani. Hizi hapa ni aina kadhaa ambazo mimi huzipendelea na ambazo naamini ni “fashionable”

No comments:

Post a Comment